Ijumaa 18 Septemba 2026 - 16:30
Madai ya Saudi Arabia Kuhusu Kulengwa Makka ni Jaribio la Kudanganya Mataifa

Hawzah/ Mahdi Muhammad al-Mashat, amesema kwamba; madai yasiyo na msingi ya utawala wa Saudi Arabia kwamba Yemen imelenga Makka, ni jaribio la kukata tamaa la kuyachochea mataifa ambayo yamefikia kiwango cha uelewa wa kutambua ukweli kuhusu utawala huo wa kihalifu.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjuma cha Shirika la Habari la Hawza, Mahdi Muhammad al-Mashat, Rais wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen, siku ya Jumatano katika taarifa yake, alisisitiza: “Madai yasiyo na msingi ya utawala wa Saudi Arabia kwamba Yemen imelenga Makka, ni jaribio la kukata tamaa la kuyachochea mataifa ambayo kiwango chao cha uelewa kimefikia kutambua ukweli wa utawala huu wa kihalifu; utawala ambao umeidhalilisha Kaaba, Qur’ani Tukufu, Misikiti Miwili Mitakatifu (Al-Haramayn al-Sharifayn), kwa kutumia mali za Umma.”

Rais al-Mashat alisema: “Wana wa Yemen wana kiwango cha juu kabisa cha imani na uaminifu kwa matakatifu ya Kiislamu, na wako tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya Nyumba Takatifu ya Mwenyezi Mungu (Baytullah al-Haram) na kuyatoa maisha yao kwa ajili yake; kama walivyoingia katika uwanja wa vita kwa ajili ya kuusaidia Msikiti wa Al-Aqsa (Haram Tukufu ya Tatu).”

Alirejelea sifa ya kipekee ya taifa la Yemen ya kujitokeza katika medani pale matakatifu ya Kiislamu yanapotukanwa, iwe ni Qur’ani Tukufu, Mtume Mkuu (saww), Makka Tukufu au Al-Aqsa Tukufu.

Rais al-Mashat alisema: “Ingekuwa bora kwa utawala huu, wakati mhalifu (Trump) alipokuwa akiidhalilisha Kaaba na kuionesha kwa namna isiyolingana na utukufu na utakatifu wake, kuhamasisha mataifa ya Umma wa Kiislamu.”

Alifafanua: “Yule aliyempa mhalifu Epstein pazia la Kaaba Tukufu kama zawadi, ndiye huyo huyo anayelenga Makka na matakatifu ya Kiislamu.”

Rais wa Baraza Kuu la Kisiasa alisisitiza: “Uongo huu hauwezi tena kuwa na athari kwa mataifa yetu ya Kiarabu na Kiislamu, kama ambavyo hapo awali madai kuhusu kutishia usafiri wa majini wa kimataifa hayakuwa na athari kwetu.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha